Dele Alli avunjika mkono wake
Imethibitishwa nyota wa Tottenham Hotspur Dele Alli alivunjika mfupa katika mkono wake wa kushoto kwenye mchezo wa robo fainali Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya Man City jumanne hii.
Licha ya uthibitisho huo wa kuvunjika baada ya kufanyiwa vipimo,timu ya madaktari ya Spurs inajaribu kutafuta njia ya kuhakikisha mchezaji huyo anacheza mechi zijazo kwa kuzingatia wameshampoteza Harry Kane ambaye ameumia kwenye kifundo cha mguu.