Onyango aitetea Uganda kwa kipigo cha Taifa Stars
Mlinda mlango namba moja wa timu ya taifa ya Uganda The Cranes Denis Onyango kwa mara ya kwanza ameongea kufuatia tuhuma dhidi ya timu yao ya taifa baada ya kupoteza kwa mabao 3-0 dhidi ya Tanzania katika mchezo wao wa mwisho wa kuwania kufuzu kucheza mataifa ya Afrika 2019 nchini Misri.
Onyango akihojiwa na Super FM akitokea Afrika Kusini katika kambi ya timu yake ya Mamelodi Sundowns kuelekea mchezo wao wa marudiano wa klabu Bingwa Afrika dhidi ya Al Ahly.
Onyango ameeleza kusikitishwa kwake na mashabiki wa Uganda baada ya timu yao kupoteza kwa mabao 3-0 dhidi ya Tanzania.
“Tumesikitishwa sana na mashabiki wetu kwa mapokeo yao. Ninafikiri mashabiki wanabidi waelewe mchezo wa mpira sio utashinda tu moja kwa moja siku zote, kama miamba ya soka kama Ujerumani na Brazil wanapoteza michezo sisi ni akina nani? Tulikuwa tukizifunga timu Namboole ina maana na hiyo ilikuwa wanapanga matokeo? “ aliseme Onyango kupitia Super FM
Hata hivyo mchezo huo umezua maneno mengi kutokana na kuwa ndio ulikuwa wa kuamua hatma ya Tanzania katika michuano hiyo ili wafuzu AFCON, kocha wa Uganda kutowachezesha wachezaji wake kama Juuko Murshid na Aucho Khalid na kuwaweka benchi kulileta maneno lakini Onyango anaungana na uamuzi wa kocha wake akisema ni maamuzi mazuri.