Eden Hazard azidi kuwatia mashaka Chelsea
Wakati mashabiki wa soka ulimwenguni wakiwa wanasubiri kujua hatma ya nyota wa kimataifa wa Ubelgji anayeitumikia klabu ya Chelsea ya nchini England Eden Hazard kujua nyota huyo ni kweli atajiunga na Real Madrid mwisho wa msimu kama tetesi zinavyosema, Hazard mwenyewe ameendelea kuacha kitendawili. .
Hazard alikuwa sehemu ya kikosi cha Chelsea ambacho kilicheza mchezo wake wa 33 wa Ligi Kuu dhidi ya majirani zao wa London West Ham United na kuwafunga kwa mabao 2-0, Hazard akifunga mabao yote hayo na kuipeleka Chelsea nafasi ya tatu kwa kuwa na alama 66 ila wamemzidi Totteham na Arsenal mchezo mmoja. .
Watu wengi wamejawa na shauku kujua mustakabali wa nyota huyo ambaye mkataba wake darajani unaisha majira ya kiangazi 2020.
.
“Kwa sasa nina malengo na Chelsea hadi mwisho wa msimu, nataka tumalize TOP 4 na Europa League, bado tuna mengi ya kufanya halafu tutaona” alisema Eden Hazard wakati wa mahojiano yake baada ya kumaliza mchezo wa Chelsea dhidi ya West Ham.
.
Hazard pia alilielezea goli lake la kwanza katika mchezo huo wa jana alieleza kuwa ni ‘Kitu fulani cha kipekee’ huku akisema kuwa ilikuwa ni vigumu kusimama kipindi anakimbia na mpira akiwa katika eneo la hatari.