Simba wakataa waamuzi kutoka Zambia
Klabu ya Simba imetuma barua ya malalamiko kwa shirikisho la soka barani Africa CAF kufuatia waamuzi wa mchezo wao wa marudiano na TP Mazembe April,13 kubadilishwa ghafla.
.
Awali waamuzi wa mchezo huo mwamuzi wa kati alikuwa anatoka Ethiopia,na mwamuzi msaidizi mmoja kutoka pia Ethiopia mwingine kutoka nchini Kenya, na Fourth Official kutoka Kenya.
.
Katika mabadiliko hayo ambayo Simba wametumiwa leo asubuhi,wakielezwa kuwa yanatokana na sababu za kiufundi,waamuzi waliopangwa ni Mzambia Janny Sikazwe ambaye ndio amepangwa mwamuzi wa kati.
Sikazwe alishawahi kuchezesha mechi ya fainali Klabu Bingwa Dunia mwaka 2016 nchini Japan kati ya Real Madrid na Kashima Anthlers, pia alichezesha mechi mbili za kombe la Dunia 2018 Russia.
.
Waamuzi wengine wote pia waliopangwa ni kutoka nchini Zambia kasoro mmoja tu ambaye ametoka Eritrea.
.
Simba wameeleza kutokubaliana na mabadiliko hayo wakisema kuwa hii inawaletea wasiwasi ukizingatia kuwa Zambia na Congo zimepakana, na ni mwendo wa kuendesha gari tu kutoka Zambia mpaka Lubumbashi.
Hivyo Simba wamewaomba CAF kuingilia kati suala hili na warudishe waamuzi waliokuwa wamepangwa hapo awali.