Santi Cazorla amwaga chozi Hispania
Ukiona mtu mzima analia,ujue kuna jambo. Kiungo wa Villarreal Santi Cazorla alimwaga chozi jana baada ya kukosa penati ambayo ingeweza kufanya wapate sare kwenye mchezo waliofungwa 2-1 na Real Betis.
Cazorla alikosa penati hiyo dakika 89 ambayo ingewapa sare na kuwaondoa katika eneo la kushuka daraja.
Villarreal sasa wanashika nafasi ya 18 katika ligi kuu nchini Hispania huku zikiwa zimebaki mechi saba msimu kumalizika.
Baada ya mchezo kumalizika, Cazorla alionekana akimwaga machozi ndani ya uwanja, na moja ya viongozi wa Villarreal akawa kumfariji.