Mfumo wa Mazembe wampa matumaini kocha wa Simba
Patrick Aussems ambaye ndio kocha mkuu wa Simba SC ameeleza kutokatishwa tamaa na matokeo ya sare ya 0-0 ya Simba dhidi ya TP Mazembe katika mchezo wao wa nyumbani, kwani ameridhishwa na uwezo wa wachezaji wake waliounesha licha ya kupoteza nafasi. .
Kutokana na kiwango walichokionesha wachezaji wake katika mchezo dhidi ya TP Mazembe ambayo ni moja kati ya timu kubwa Afrika, anaamini kwa mfumo wanaocheza Mazembe wa kucheza mpira basi Simba wakienda Lubumbashi wanaweza kucheza na kufuzu nusu fainali.
.
“Nimeridhishwa na wachezaji wangu na najivunia wao kwa sababu wameonesha kiwango mbele ya timu kubwa kama TP Mazembe, tulikuwa na nafasi nyingi tulistahili kufunga lakini tumekosa penati hivyo vitu vinatokea katika mchezo, ndio maana hata TP Mazembe wanafurahi wanarudi Congo na sare , wiki ijayo nina uhakika tunaweza kufunga na kufuzu na uhakika kwa sababu TP Mazembe ni timu inayocheza mpira” alisema Aussems mbele ya waandishi baada ya mechi.
Jumamosi ijayo,April 13 mjini Lubumbashi,Congo ndio mechi ya marudiano kati ya timu hizo itapigwa.