Paul Ince haamini kama Pogba ataendelea kuwepo Man United
Nyota wa zamani wa Manchester United Paul Ince ameeleza mtazamo wake kuhusiana na hali iliyopo kwa sasa katika klabu ya Manchester United kuhusiana na habari za Paul Pogba kudaiwa kuwa anaweza akahama mwisho wa msimu na kujiunga na Real Madrid kama ambavyo inaripotiwa.
Paul Ince amemshauri kocha mkuu wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer kumshauri na kumshawishi Paul Pogba asiondoke katika klabu hiyo.
Pamoja na kupata nafasi katika utawala wa Solskjaer ila Paul Ince hafikiri kama Pogba atabakia Man United mwisho wa msimu.
.
“Ole anatakiwa kumshawishi Pogba kuwa anakwenda kuitengeneza timu kumzunguuka yeye, kama anamtaka abakie Man United, kiukweli sifikirii kama Paul Pogba atabakia Old Trafford msimu ujao” alisema Paul Ince
Ince anasema kuwa ni vigumu sana kumbakiza mchezaji kipindi Real Madrid wanapokuwa wamebisha hodi.