Kocha wa Simba abeba Tuzo ligi kuu
Kamati ya Tuzo imemchagua Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems kuwa Kocha Bora wa Machi akiwashinda Kocha Mkuu wa Azam, Abdul Mingange na Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar, Zuberi Katwila.
Hii ndio mara ya kwanza kwa Kocha huyo kuweza kuchaguliwa kuwa Kocha bora wa mwezi tangu alipojiunga na Klabu ya Simba Julai 19 mwaka 2018.
Katika mwezi huo Simba SC ilishinda michezo yote mitatu iliyocheza na ikiwa inashika nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi hiyo.
Kocha Aussems atazawadiwa Tsh 1,000,000 (milioni moja) na tuzo kutoka Biko Sports ambao ndio wadhamini wa Tuzo hizo.