Siku za Courtois Madrid zinahesabika
Kocha Zinedine Zidane alivyoondoka Real Madrid baada ya msimu uliopita kuisha,timu hiyo ikamsajili kipa Thibaut Courtois kutoka Chelsea akaja kuchukua nafasi ya Keylor Navas golini.
Baada ya Zidane kurejea Real Madrid mwezi uliopita,mechi yake ya kwanza akamrudisha Keylor Navas golini, huku Courtois akikaa benchi.
Courtois amekuwa na wakati mbaya katika msimu wake wa kwanza Real Madrid, akicheza katika kiwango cha chini.
Kwa maneno ya Zizou leo katika mkutano na waandishi wa habari, imeripotiwa kuwa tunaweza kushuhudia kipa huyo wa kimataifa wa Belgium akiuzwa katika majira ya kiangazi mwaka huu.
.
“Ninawapa uhakika kuwa mwakani kutakuwa hakuna mjadala kuhusu kipa.”
.
“Ninawaambia sasa hivi.(Kila kitu) kinaenda kuwa wazi kabisa” amesema Mfaransa huyo leo.