Pochettino ampa sifa beki wa Liverpool
Kocha wa Tottenham Hotspur Maurcio Pochettino amesifia uwezo wa beki wa Liverpool Virgil van Dijk aliounesha jana katika mechi ambayo majogoo hao waliondoka na ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Spurs Anfield.
Pochettino amesifia namna ambavyo beki huyo aliweza kumzuia mchezaji wake Moussa Sissoko asifunge katika dakika za mwisho wa mchezo muda mchache kabla ya Liverpool kupata goli la ushindi kupitia kwa
beki Toby Alderweireld ambaye alijifunga.
.
“Hiyo inaonesha kwa nini Liverpool Liverpool walilipa zaidi Pauni Milioni 70 kwa Van Dijk” Pochettino aliiambia Sky Sports
Van Dijk alipata sifa nyingine kutoka kwa mchezaji mwenzake wa Liverpool, beki Trent Alexander-Arnold ambaye alimfisia kuwa ni beki bora duniani.
.
“Van Dijk ameonesha tena kwa nini yeye ni beki bora duniani”