Yakubu Mohammed hajatua msimbazi, ni mali ya Azam
Zimeenea habari katika mitandao ya kijamii kuwa klabu ya wekundu wa Msimbazi Simba SC imemalizana na beki wa kati wa kimataifa wa Ghana Yakubu Mohamed ambaye kwa sasa anaitumikia klabu ya Azam.
Msemaji wa Azam FC Jaffary Iddi ameweka wazi kuwa hakuna ukweli wowote katika habari hiyo zaidi mchezaji huyo ni wao na taratibu za mchezaji kutoka timu moja kwenda nyingine zinajulikana hivyo hakuna ukweli wowote katika tetesi hizo. .
“Napenda kutamka rasmi mchezaji Yakubu Mohamed ni mali ya Azam FC, kumekuwa na taarifa kwa baadhi ya vyombo vya habari kumuhusisha mchezaji huyo kwenda Simba SC, tunatoa onyo kwa chombo chochote kitakachotoa taarifa hiyo pasipo ku-balance, mwanasheria wetu ataweza kuchukua hatua kali” alisema Jafari Iddi Maganga
Azam FC waliopo katika nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania bara nyuma ya Yanga wanaoongoza , wameonekana kuzidi kudhibiti na kuhakikisha mchezaji aliyekuwa na mchango katika kikosi chao haondoki na ndio maana katika kipindi cha siku 14 wamewaongezea mkataba Donald Ngoma, Bruce Kangwa na Abdallah Kheri.