Solskjaer aitajirisha Molde FC
Klabu ya Man United imeilipa kiasi cha Pauni Milioni 1 (Tsh (Bilioni 3) klabu ya zamani ya kocha Ole Gunnar Solskjaer, Molde ya Norway baada ya kocha huyo kusaini mkataba wa kudumu wa miaka mitatu Old Trafford.
Imeripotiwa kuwa Man United imeilipa pesa hizo timu hiyo ikiwa ni ishara ya shukurani kwa kumchukua kocha huyo na pia kujenga uhusiano mzuri baina ya timu hizo.
Imeelezwa kuwa Molde walilipwa nusu ya hela hiyo mwezi Disemba mwaka jana Solskjaer alipochukuliwa kuwa kocha wa muda wa Man United,na sasa mashetani hao wamemalizia nusu iliyobaki baada ya jana kumpa kocha huyo mkataba wa kudumu wa miaka mitatu wenye thamani ya takribani Pauni milioni 21.