Amunike akanusha kumpa kazi Okocha
Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Mnigeria Emmanuel Amunike amejibu tetesi zilizokuwa zimeenea kuwa ameamua kumuongeza mnigeria mwenzake Jay Jay Okocha kama kocha msaidizi wake kuelekea fainali za mataifa ya Afrika 2019.
Taarifa zinakuja zikiwa zimepita siku nne tokea Tanzania ifanikiwa kufuzu kucheza fainali za mataifa ya Afrika 2019 kwa mara ya kwanza baada ya kushindwa kwa miaka 39 kupata tiketi hiyo, hivyo zikazusha tetesi kuwa Amunike ameamua kuboresha benchi lake la ufundi.
Akihojiwa na TBC 1 Amunike ameweka wazi na kukanusha tetesi hizo na kusema kuwa hawezi kumchukua Okocha kwa sababu sio kocha kwa sasa “Okocha sio kocha wala simtafuti kocha mpya na hata kama nina mpango wa kuongeza watu watakuwa wanaongeza kitu timu ya taifa, sasa Okocha sio kocha unawezaje kumleta. Sio kweli watu wanapenda kuongea na kila mtu yupo huru kuongea anachopenda na kutoa maoni yake”