Man City na Liverpool ni bora kuliko Barca
Kocha wa zamani wa Manchester United Lous van Gaal pamoja na kuwa ameachana na kazi ya ukocha na kuamua kupumzika na kuendelea na maisha mengine, hiyo haimaanisha huwa hachangii chochote kuhusu mchezo wa soka.
Louis van Gaal ameenda tofauti na wadau na wachambuzi wengi ambao wamekuwa wakiamini na kuitaja klabu ya FC Barcelona ndio klabu bora duniani, Van Gaal kwa upande wake anaona timu bora kwa sasa ngazi ya vilabu ni Manchester City na Liverpool. .
“Watu wanafikiri Barcelona ndio bora lakini sio, Man City na Liverpool ni zaidi ya timu kwa sasa na Liverpool ndio bora zaidi ya Manchester City” alisema Louis van Gaal katika mahojiano yake na BBC Sports
Bado haijajulikana Louis Van Gaal ametumia kigezo kipingi kuzitaja Manchester City kama ndio klabu bora.