Chicharito afunga ndoa kwa siri California
Imethibitika kuwa nyota wa West Ham United Javier Hernandez ‘Chicharito’ amefunga ndoa kwa siri na mpenzi wake Sarah Kohan ambaye ni mwanamitindo maarufu katika mtandao wa Instagram.
Mwanadada huyo mwenye umri wa miaka 24, raia wa Australia ana mimba ya miezi saba ya mchezaji huyo wa zamani wa Man United.
Sarah Kohan amethibitisha kuwa wameoana na Mmexico huyo kwa siri huko Chula Vista,California wiki iliyopita. .
‘ Ndio tumeoana .Hakuna cha kuficha.Wikiendi njema kwa kila mmoja.’ Aliandika Sarah katika mitandao ya kijamii.
Chicharito na Sarah ambaye pia ni mhitimu wa sheria katika chuo cha Havard wanataraji kupata mtoto wa kiume ambaye atakuwa ni mtoto wao wa kwanza wakiwa pamoja.