Yanga yapigwa faini ya milioni 6
Kamati ya uendeshaji na usimamizi wa Ligi ijulikanayo kama kamati ya saa 72 ,imeitoza faini ya jumla ya sh.milioni 6 Klabu ya Yanga kwa makosa mawili , ya kuingia Uwanjani kwa kutumia mlango usio rasmi pia kwa kutoingia vyumbani wakati wa mapumziko katika mchezo wa Ligi kuu Tanzania bara dhidi ya KMC, uliochezwa Machi 10 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, ambapo katika mchezo huo Yanga ilishinda bao 2-1.
Mtendaji mkuu wa Bodi ya Ligi Boniface Wambura amesema kuwa wakati kamati imechukua maamuzi hayo imefuata kanuni na kwa sasa Klabu zitakazo fanya makosa kama haya yakujirudia rudia zitatozwa faini ya milioni 3 na sio laki 5 kama ilivyozoeleka na Klabu ya Yanga ni mara ya tatu kufanya kosa hilo katika mechi za Ligi kuu Tanzania bara msimu huu wa 2018/2019