McGregor atundika daruga UFC
Nyota wa UFC kutoka Ireland Conor McGregor leo Machi 26 kupitia mtandao wa twitter ametangaza kustaafu mchezo wa Mixed Martial Art (MMA) akiwa na umri wa miaka 30.
McGregor anaondoka katika mchezo huo akiwa amepigana mapambano 25, ambapo ameshinda 21 na kupoteza mara 4.
Pambano lake la mwisho kushuka katika Octagon lilikuwa Oktoba 6,2018 ambapo alipigwa katika raundi ya nne na Mrusi Khabib Nurmagomedov