FIFA yataja tarehe ya kusikiliza rufaa ya Chelsea
Tarehe 22 Februari mwaka huu shirikisho la mchezo wa mpira wa miguu duniani (FIFA) lilitangaza kuiadhibu Chelsea kwa kuifungia madirisha mawili kufanya usajili, FIFA baada ya Chelsea kukata rufaa imethibitisha kuwa rufaa ya Chelsea dhidi ya adhabu hiyo itasikilizwa na April 11 2019.
Tukukumbushe tu FIFA iliifungia Chelsea kufanya usajili wa kwa kipindi cha usajili wa madirisha mawili, baada ya kubaini kuwa wamefanya usajili wa wachezaji wenye umri chini ya miaka 18 kinyume na sheria zinavyotaka.
Chelsea walikumbana na adhabu hiyo baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kubainika na hatia ya matukio 29 ya kuvunja ibara ya 19 ambayo inahusiana na usajili wa wachezaji chini ya miaka 18.
Kuachana na adhabu hiyo ya kufungiwa kufanya usajili pia the blues walipigwa faini ya pauni 460,000.