UEFA yamshitakk Neymar
Mchezaji wa PSG Neymar Jr ameshitakiwa na shirikisho la soka barani Ulaya UEFA kwa maneno yake aliyotoa dhidi ya waamuzi wa mchezo wa timu yake dhidi ya Man United Machi 6, ambapo mechi hiyo iliisha kwa United kushinda goli 3-1 na kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano ya klabu Bingwa.
Goli la penati la Marcus Rashford dakika za mwisho ndio lililoipelekea Man United robo fainali, na ndio goli hilo ambalo lilifanya Neymar kupitia account yake ya Instagram kutoa maneno makali dhidi ya waamuzi “ Hii ni fedheha, wanawaweka watu wanne wasiojua chochote kuhusu mpira katika kuangalia marudio ya VAR” aliandika hivyo Neymar ambaye alikosa mechi hiyo kutokana na kuwa majeruhi.
Kesi yake itajadiliwa na kamati ya nidhamu ya UEFA, lakini tarehe ya kusikilizwa kwa kesi hiyo bado haijatajwa.
Mchezaji huyo anaweza kupigwa faini au kufungiwa mechi moja mpaka tatu na shirikisho hilo.