Pogba awatia mashaka Man United
Wakati Paul Pogba akiwa katika kambi ya timu yake ya taifa ya nchini Ufaransa kwa ajili ya michezo ya kuwania kufuzu kucheza michuano ya euro, imetoka taarifa kuhusiana na kauli yake kuwa inachochechea au wapa matumaini Real Madrid waongeze bidii ya kumuhitaji kwa kutuma ofa Manchester United.
Katika mkutano wa waandishi wa habari huko France Paul Pogba amaeulizwa kuwa kama anaweza kuwa sehemu ya kikosi cha Real Madrid au anatamani kuichezea timu hiyo, ameweka wazi kuwa Real Madrid ni klabu ya ndoto ya kila mchezaji kucheza, kauli hiyo inaweza ikawapa nguvu Real Madrid kuwa inaweza kumpata kama watamuhutaji na kutoa ofa za maana.
“Siku zote nimekuwa nikijibu hivi, Real Madrid ni ndoto ya kila mmoja ,ni moja kati ya klabu kubwa duniani.
Pia Zinedine ni kocha pale na ni ndoto ya yoyote anayependa soka” alisema Paul Pogba
aliyedaiwa kutoa kauli ya kuwapa baraka Real Madrid
.
“Kwa sasa nipo Manchester. Hatujui mbeleni kuna nini. Nipo Manchester na ninafuraha” aliongeza Paul Pogba.
Mfaransa huyo amebakiza miaka miwili katika mkataba wake na Man United na sasa ni mchezaji mwenye furaha akiwa chini ya kocha Ole Gunnar Solskjaer.