Giggs amjibu Zlatan
Zlatan Ibrahimovic aliamua kuwatolea uvivu wakongwe wa zamani wa Manchester United Ryan Giggs, Paul Scholes pamoja na mwenzao Gary Neville ambao kwa sasa awamekuwa wakifanya kazi za uchambuzi wa soka katika vituo vya TV, ukosoaji wa manguli hao umewafanya Zlatan aamua kuwapiga dongo.
Kutokana na aina ya uchambuzi wao wa kusema na kukosoa baadhi ya wachezaji kama Paul Pogba, Zlatan amewapiga kijembe kuwa kama wanataka kazi Manchester United wanabidi wakaombe na sio kukosoa kosoa tu kwenye TV wakati muda wao wa kucheza soka ulishaisha.
Ryan Giggs amejibu nae kwa kauli inayotafsirika kama kejeli kwa Zlatan kwa kusema kuwa “Sisi ni mashabiki wa timu, pamoja na wachezaji wengine wa zamani ambao wapo kwenye TV au Redio.
Ndivyi mpira ulivyo, kuwa na mawazo tofauti tofauti. Lakini labda inawezekana (Zlatan) anaijua sana Klabu zaidi yetu sisi” alisema Ryan Giggs ambaye amedumu na Manchester United kwa miaka 24 kama mchezaji na Zlatan amecheza Manchester United kwa miaka miwili.