Makamba mgeni rasmi mechi ya Simba na AS Vita
Kikosi cha wachezaji walioitwa katika Timu ya Taifa ya Tanzania ” Taifa stars ” kinatarajia kuingia kambini Machi 17 mwaka huu ( jumapili) kwenye hotel ya seascape iliyopo mbezi beach Dar es Salaam kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa kuwania kufuzu fainali za AFCON dhidi ya timu ya Taifa ya Uganda
Katika mchezo huo utakaochezwa Machi 24 mwaka huu saa 12.00 jioni kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam,Tanzania inahitaji kushinda katika mchezo huo ili kujitengenezea mazingira ya kufuzu kucheza fainali za Kombe la mataifa Afrika AFCON
Msemaji wa Shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF), Clifford Mario Ndimbo amesema kuwa Kikosi kilichoitwa na Kocha mkuu Emmanuel Amunike kitaanza mazoezi yake Machi 18, hii ni baada ya wachezaji kuwasili kambini wakitokea katika timu zao.