MESUT OZIL KAONESHA MAPENZI KWA DOGO WA KENYA
Kiungo wa klabu ya Arsenal ambaye pia ni mjerumani mwenye asili ya Uturuki Mesut Ozil, baada ya kuenea na kusambaa kwa picha ya mtoto Lawrence kutokea nchini Kenya amevaa jezi ya Arsenal iliyoandikwa kwa mkono jina la Mesut Ozil, nyota huyo ameonesha kuguswa.
Picha hiyo ya mtoto huyo akichunga ng’ombe ikiwa imesambaa mitandaoni, ilimuonesha mtoto huyo katika mitandao mbalimbali ya soka duniani kiasi cha Ozil kuamua kuguswa na kumtumia mtoto huyo jezi yake, viatu vya Adidas pamoja na kofia.
Kwa kawaida hususani barani Ulaya kwa shabiki wa soka kumiliki jezi Orijino ya mchezaji ampendae ni fahari na huwa ina thamani kubwa kuliko ya kwenda kuinunua dukani, hivyo Ozil kwa kuthamini upendo wa mtoto huyo ametumia gharama na kuzisaini jezi za mtoto huyo na kumtumia nchini Kenya.