KIBALI CHAMKWAMISHA AMBOKILE KUCHEZA KATIKA TIMU YAKE
Mshambuliaji wa Klabu ya Mbeya city ambae kwa sasa yupo katika timu ya Black Leopard ya Afrika kusini kwa majaribio tangu January 30 mwaka huu alipojiunga na Klabu hiyo amesema kuwa kwa sasa tayari ameishaimarika kucheza katika timu yake kinachosubiriwa ni kibali tu cha kumruhusu yeye kuanza kucheza.
Mshambuliaji huyo mpaka anaondoka katika timu yake ya Mbeya City alikuwa anashika nafasi ya juu kati ya wachezaji wenye wastani wa magoli mengi katika ligi kuu Tanzania Bara akiwa ameifungia timu yake magoli 10.
“Namshukuru Mungu naendelea vizuri huku na tayari nimeishaimarika kuanza kuichezea timu yangu ninachosubiri ni kibali tu,nafikiri mpaka tarehe 29 kibali kitakuwa tayari na nitaanza kucheza maana kwa sasa Ligi ya huku imesimama mpaka Machi 29 mwaka huu”amesema Ambokile wakati akizungumza na #WorldSports14 kwa njia ya simu.

Ambokile pia amesema kuwa anayafurahia maisha ya kisoka ya nchini Afrika kusini na anataraji kucheza nchini humo misimu mingi sana.
.
” Nayafurahia sana maisha ya huku kwa sababu Ligi yao ni bora sana na viongozi wanaheshimu sana kazi za wachezaji na wachezaji pia wanaheshimu pia kazi zao .
Na utofauti wa Soka la nyumbani na huku ni mkubwa sana itachukua muda sana nchi yetu kuweza kufikia katika level ya huku” amesema mchezaji huyo.