Solskjaer kulipwa mshahara nusu wa Mourinho
Pamoja na kuwa klabu ya Manchester United ilimtangaza kuwa Ole Gunnar Solskjaer ni kocha wa muda wa klabu hiyo hadi mwisho wa msimu watakapoamua kumtangaza nani kocha wa kudumu baada ya kumfuta kazi Jose Mourinho mwezi Desemba 2018, inaonekana Solskjaer kama ndio bahati itamuangukia.
Mitandao mbalimbali habari za michezo barani Ulaya kufuatia kufanya vizuri kwa Ole Gunnar Solskjaer wamekuwa wakimtabiria kupewa ajira ya kudumu ndani ya Old Trafford, inaelezwa kuwa kuna kila dalili kuwa Solskjaer anaweza kuwa kocha mkuu wa Manchester United mwisho wa msimu baada ya matokeo ya timu hiyo kuivutia bodi ila ishu ni mshahara.
Habari kutoka ndani ya bodi ya wakurugenzi wa klabu hiyo zilizoripotiwa na ITV Sports zinaeleza kuwa licha ya Ole Gunnar Solskjaer kupandisha kiwango cha Manchester United kwa kasi toka aanze kuifundisha timu hiyo, uongozi umeridhia kumpa mkataba ila unataka kumlipa nusu ya mshahara aliyokuwa analipwa kocha wao aliyepita Jose Mourinho.
Mourinho licha ya kuboronga siku za mwishoni akiwa na Manchester United alikuwa akilipwa mshahara wa pauni milioni 20.7 kwa mwaka, Ole Gunnar Solskjaer hadi sasa ameifanikisha Manchester United kuiingiza TOP 4 ikiwa na alama 58 katika Ligi Kuu ya nchini England kitu ambacho ilidaiwa kuwa timu ingeendelea kuwa chini ya Mourinho ingezidi kushuka.