Rais wa Madrid amkataa Jose Mourinho
Baada ya kuzuka kwa uvumi kuwa Real Madrid ipo mbioni kumrudisha kocha wake wa zamani mreno Jose Mourinho ambaye hana timu kwa sasa toka apoteze ajira yake kwa matokeo mabovu ndani ya Manchester United mwezi Desemba 2018, Rais wa zamani wa Real Madrid hajakubaliana na hilo.
Ramon Calderon ambaye ni Rais wa zamani wa Real Madrid ameeleza hakubaliani na Jose Mourinho aliyewahi kuifundisha timu yao kwa miaka mitatu kuanzia 2010.

Ramon anasisitiza mreno huyo asirudi Bernabeu kwani alisababisha madhara makubwa katika timu yao.
“Kurudi kwa Mourinho? Kiukweli hapana tayari nimeshaorodhesha idadi ya mambo mabaya aliyowahi kuyasababisha hapa, mtindo wake wa uchezaji sio aina ya mchezo ambao Bernabeu inataka, kitu mashabiki wanachokitaka ndio hicho hicho wanachotakiwa kukipata kama ambavyo umeona kutoka kwa Ajax “ alisema Rais wa zamani wa Real Madrid Ramon Calderon akihojiwa na ESPN
Real Madrid toka waondoke Cristiano Ronaldo kwenda Juventus na kocha wao Zinedine Zidane kujiuzulu baada ya kushinda mara tatu taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya, wamekuwa na wakati mgumu kiasi cha kuondoka katika mbio za kuwania taji lolote msimu huu baada ya kuondolewa pia katika 16 bora na Ajax katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.