Alliance wafurahi kukutana na Yanga tena
Ikiwa ni siku kadhaa zimepita tangu Yanga kuibuka na ushindi wa 1-0 ugenini dhidi ya Alliance katika mchezo wa Ligi kuu , timu hizo zimepangwa kukutana tena kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho la Azam Sports Federation Cup ambapo Alliance ndio mwenyeji wa mchezo huo.
Droo hiyo ya robo fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho imefanyika leo na timu zimepangwa kukutana.
Worldsports14 imemtafuta msemaji wa Klabu ya Yanga Dismas Ten baada ya droo hiyo kupangwa “Hilo halina mjadala kwa sababu droo ishachezeshwa na tumepangwa na Alliance FC tutaenda kucheza na kuhakikisha tunafanya vizuri katika mchezo huo ili kuhakikisha tunaingia hatua ya nusu fainali na fainali pia? amesema Ten
“Hilo halina mjadala kwa sababu droo ishachezeshwa na tumepangwa na Alliance FC tutaenda kucheza na kuhakikisha tunafanya vizuri katika mchezo huo ili kuhakikisha tunaingia hatua ya nusu fainali na fainali pia? amesema Ten
Kwa upande wa Alliance kupitia kwa Mwenyekiti wa kamati ya mashindano Yusuph Budodi ameonesha kufurahi kukutana na Yanga tena, na kueleza kuwa hawaihofii Yanga maana ni timu ya kawaida na watashinda katika mchezo huo.
.
” Nilikuwa na hamu sana tukutane na Yanga tena kutokana na mambo yaliyotokea katika mchezo wetu wa Ligi kuu ,Mungu ni mwema droo imechezeshwa na tunakutana tena. Yanga ni timu ya kawaida, ni timu Kongwe lakini uwanjani ni timu ya kawaida na tutafanya vizuri katika mchezo huo wa FA na tutawafunga na kitinga nusu fainali “amesema Budodi
Pia katika michuano hiyo Lipuli FC atakuwa mwenyeji wa Singida United, KMC atakuwa mwenyeji wa Afrika Lyon na Kagera Sugar atakuwa mwenyeji wa Azam FC.