Mnyama kuwafuata Waarabu kesho
Baada ya kurejea Leo Jijini Dar es Salaam kutokea mkoani Shinyanga kilikokuwa na mchezo wa ligi kuu Tanzania bara, Kikosi cha Simba kinatarajia kuanza safari kesho ya kuelekea nchini Algeria kwaajili ya mchezo wa Klabu Bingwa Afrika dhidi ya JS Saoura.
Mchezo huo utakaowakutanisha Mabingwa hao utachezwa machi 9 mwaka huu nchini Algeria.
#Worldsports14 imemtafuta Meneja wa Klabu hiyo Patrick Rweyemamu amesema kuwa Kikosi kimewasili salama Jijini Dar es Salaam na kesho kinaanza safari ya kuelekea nchini Algeria kwaajili ya mchezo huo

” Tunashukuru Mungu kwa ushindi tulioupata jana na tumerudi salama nyumbani na leo tutapata mapumziko,kesho saa kumi za jioni tutaanza safari yetu ya kwenda nchini Algeria kwaajili ya mchezo wetu dhidi ya JS Saoura tutakao cheza machi 9 mwaka huu”amesema Patrick

Simba SC anakutana na JS Saoura akiwa anashika nafasi ya pili katika msimamo wa kundi D akiwa na point sita,huku Saoura akishika nafasi ya tatu akiwa na point tano.