Mario Balotelli amekuja na balaa jipya
Mshambuliaji wa zamani wa timu za Inter Milan, Manchester City na Liverpool anayecheza Olympique Marseille kwa sasa Mario Balotelli bado anaendelea na vituko vya katika soka, licha ya kuwa Balotteli anakipaji cha hali ya juu amekuwa na tabia ya kupenda kufanya vitu vya kipekee wakati mwingine vinachekesha na mwingine vinamuweka matatani na makocha wake.
Akiwa sehemu ya mchezo wa Marseille dhidi ya Saint Etienne wa Ligi Kuu ya nchini Ufaransa ambayo ni maarufu kama Ligue 1, Balotelli katika mchezo huo wa 27 wa timu yake alifanikiwa kufunga bao la kwanza dakika ya 12 katika ushindi wa Marseille wa 2-0 kwenye mchezo huo.
Gumzo la Balotelli mwenye umri wa miaka 28 katika mchezo huo ilikuwa ni staili yake ya kushangilia goli hilo ambaoo alikwenda kuomba simu ya mkononi kwa mpiga picha , kisha kuanza kujirekodi video na wachezaji wenzake wakishangilia,na kui-post video hiyo kwenye insta story ya Instagram yake na kurudi uwanjani kuendelea na mechi.
Hilo ni bao la nne kwa Balotelli akiichezea Marseille katika mechi 6 za Ligue 1 toka ajiunge nayo mapema mwezi Januari mwaka huu akitokea Nice, Marseille kwa sasa wapo nafasi ya nne katika msimamo wa Ligue 1, wakiwa nyuma ya Lyon waliopo nafasi ya tatu kwa kuwa na alama 49 wakiwazidi Marseille alama 5, Marseille wao wana alama 44.