Icardi achoshwa na Inter Milan
Kuna kila dalili mshambuliaji wa kiargentina anayecheza Inter Milan Mauro Icardi amechoshwa na maisha ya Inter Milan na huenda akataka kuondoka mwisho wa msimu.
Sekeseke la Mauro Icardi kutokuwa na raha Inter Milan lilianzia pale ambapo alipovuliwa kitambaa cha unahodha ambacho amekuwa kiongozi Inter Milan kwa muda.
Icardi kwa kauli anazozitoa hadharani haziashirii kwamba anatazamia kuwa na mazungumzo na kuendelea kuitumikia timu hiyo, kwani ameshatoa kauli za kuwa Inter Milan hakuna upendo wa heshima, Mauro Icardi toka avuliwe unahodha hajaichezea timu hiyo kwa mechi nne na anataraji kuukosa mchezo wa tano dhidi ya Cagliari Ijumaa hii.
Kwenye ujumbe ambao ameuandika katika mtandao wa Instagram, Icardi amesisitiza kuwa amekuwa na Inter Milan katika kila hali na matatizo yote, muda mwingine akicheza akiwa na maumivu lakini hakujali kutokana na mapenzi yake na heshima kwa klabu.
Mshambuliaji huyo mwishoni mwa ujumbe huo anasema hajui kama sasa heshima na upendo huo upo kwa Inter na kwake.
“Sijui kama kwa sasa kuna upendo na heshima kwa Inter Milan na kwangu mimi kwa kufuatana na baadhi ya watu ambao wanafanya maamuzi”
Icardi kwa sasa ana miaka sita akiwa na Inter Milan toka alipojiunga na timu hiyo 2013 akitokea Sampdoria na ameonesha kutotaka kuendelea na timu hiyo akiwa na umri wake wa miaka 26 baada ya kuandika ujumbe huo mrefu kupitia ukurasa wake wa instagram
Kocha wa Inter Milan Luciano Spalletti amesisitiza kuwa hawezi kuzungumzia sana suala la Icardi kwani tayari alishaongea na uongozi wa juu ulishaongea.
Hata hivyo CEO wa Inter Milan Beppe Marotta alinukuliwa na vyombo vya habari mapema wiki hii kuwa tayari wameshaongea na wakala wa Icardi ambaye ni mke wake Wanda Nara kuwa wana ofa ya kumuongezea mkataba Icardi japo hawana imani kama itakubaliwa.