Cardiff wathibitisha hawakumtekeleza Sala
Baada ya kubainika kuwa mshambuliaji mpya wa Cardiff City Emiliano Sala aliyepoteza maisha katika ajali ya ndege Januari 21 akiwa na rubani wake David Ibbotson kuwa ndege aliyokuwa anaitumia kusafiria kutokea Nantes kuelekea Cardiff City nchini Wales haikuwa imesajiliwa kubeba abiria mengi yamekuwa yakiibuka.
Mtandao wa daily mail umeripoti kuvuja kwa meseji za whatsapp za Cardiff City kuhusu kumpa ofa Emiliano Sala ya usafiri wa ndege lakini mchezaji huyo alikataa baada ya wakala wake McMakay kudai kuwa klabu hiyo imemtelekeza hivyo usafiri wa kurejea Cardiff City ataandaa mwenyewe.
Meseji hizo za Whatsapp zilizofuja zinaonesha Afisa mmoja wa klabu ya Cardiff akimpa jina la ndege ambayo anatakiwa apande ambayo itapitia Paris, lakini Emiliano akamwambia Afisa huyo kuwa tayari wakala Willie McKay alishamtafutia ndege ya kusafiri nayo.
Mfululizo wa meseji hizo zilizovuja zinaeleza kuwa kuwa Emiliano Sala hakuwa ametelekezwa na Cardiff City katika suala zima la kutafutiwa usafiri kama wakala wake Willie McKay alivyodai kuwa baada ya kusaini mkataba wa kuichezea Cardiff City, klabu hiyo haikumtafutia usafiri mchezaji huyo kitu ambacho kilipelekea aandae mwenyewe taratibu za usafiri zilizopelekea kifo chake.
Akihojiwa na BBC wakala wake McKay alisema “alitelekezwa hotelini kiasi cha kufikia hatua ya kuandaa usafiri wake mwenyewe, hakuna mtu yoyote Cardiff alikuwa akionekana anafanya chochote kwa ajili yake, wamemnunua mchezaji kwa pauni milioni 15 halafu wanamtelekeza mchezaji hotelini anaanza kuangahika na computer kutafuta ndege mwenye”
.
Emiliano Sala siku mbili kabla ya kifo chake alifanikiwa kusaini mkataba wa miaka mitatu wa kuitumikia Cardiff City ya nchini Wales kwa ada ya uhamisho wa pauni milioni 15 akitokea Nantes FC ya nchini Ufaransa, hivyo akakodi ndege kutoka Cardiff kurudi Nantes baada ya kusaini mkataba wake kwa ajili ya kuwaaga wachezaji wenzake wa zamani ila wakati anarudi Cardiff baada ya kumaliza kuwaaga wachezaji wenzake ndio akapata ajali akiwa katika ndege ndogo ya injini moja akiwa yeye (Emiliano Sala) na rubani wake (David Ibbotson)