Terry ataja siri ya kutobadili jezi yake Chelsea
Legend na nahodha wa zamani wa klabu ya Chelsea yanchini Uingereza John Terry ambaye ana umri wa miaka 38 kwa sasa akiwa kastaafu kucheza soka, ameamuakuweka wazi kwa nini aliamua kutumia namba 26 katikamaisha yake ya soka kwa muda wote akiwa katika klabuyake ya Chelsea. John Terry ambaye ameanza kuichezea Chelsea tokatimu za vijana mwaka 1995 hadi alipopandishwa 1998, alikuwa akiitumia jezi namba 26 kwa sababu aligunduamapema tu kuwa alikuwa na mashabiki hata kabla yakuanza kupata nafasi katika kikosi cha kwanza ndipoalipoona asibadili jezi atawatia hasawa mashabiki wake kununua jezi mpya. “Nilipopata nafasi ya kuingia katika kikosi cha kwanza cha Chelsea na kuanza kuchez, hiyo ndio ilikuwa nambayangu ya jezi (26) nilikuwa nimeona baadhi yamashabiki wakiwa wamevaa jezi yangu yenye jina languna namba yangu, sikutaka kubadili namba kwa sababusikutaka niwape hasara ya kununua jezi nyingine” alisema John Terry. John Terry amekuwa ni moja kati ya mabeki bora wa katiwa klabu ya Chelsea kuwahi kutokea na amedumu katikatimu hiyo kwa miaka 9 toka 1998-2017 ila aliwahikwenda kwa mkopo katika klabu ya Nottingham Forest mwaka 2000 kabla ya kuamua kumaliza soka lake akiwana Aston Villa msimu wa 2017-18 na sasa kochamsaidizi wa timu hiyo inayoshiriki Championship nchiniUingereza (Ligi daraja la kwanza)