Yanga wanazitaka Pointi 3 kwa Alliance
Kikosi cha Yanga Sc kimewasili jijini Mwanza tayari kwa mchezo ujao wa Ligi Kuu dhidi ya Alliance FC utakaochezwa katika Uwanja wa CCM Kirumba Jumamosi hii Machi 2
Msemaji wa Klabu hiyo Dismas Ten amesema kuwa wachezaji 20 na viongozi 8 tayari wameisha wasili Jijini mwanza kwaajili ya mchezo huo.
Ten amesema kuwa mchezo huo utakuwa mchezo mgumu ukiangalia Alliance FC ni Timu nzuri na inaendelea kufanya vizuri katika mechi zake za Ligi kuu Tanzania bara.
” Mchezo wetu dhidi ya Alliance hapo jumamosi utakuwa mchezo mgumu, Alliance ni Timu nzuri ina wachezaji wazuri hivyo tumeenda kwa tahadhari na tutahakikisha tunapata ushindi katika mechi hiyo na kurudi na point tatu nyumbani “ amesema Ten.
Yanga anakutana na Alliance FC akiwa amecheza michezo 25 na kushika nafasi ya kwanza katika msimamo wa Ligi kwa kuwa na point 61 huku Alliance akiwa amecheza michezo 28 nakushika nafasi ya 7 na kuwa na point 36