Ranieri atimuliwa Fulham
Kocha Claudio Ranieri amefutwa kazi katika klabu ya Fulham ikiwa imepita miezi mitatu tangu ajiunge na timu hiyo.
Scott Parker ametangazwa kuwa meneja wa muda kwa sasa.
Fulham imeshinda mechi tatu tu kati ya 17 chini ya kocha Claudio Ranieri, na timu inashika nafasi ya 19 kwenye msimamo wa ligi kuu nchini England.