Ramos alichowaambia wenzake jana katika mechi ya Barca
Baada ya Barcelona kunako dakika ya 73 kuwa mbele kwa goli 3-0 jana Santiago Bernabeu katika mechi ya pili ya nusu fainali Copa del rey dhidi ya Real Madrid, Ramos alionekana akiwaambia wachezaji wenzake
“Come on, tusiwaache watufunge sita, come on”.
Pengine kauli hiyo ilisaidia kwani baada ya hapo hawakuruhusu kufungwa goli lingine tena, na mechi ikaisha kwa Barca kushinda kwa goli 3-0 na kufuzu hatua ya Fainali ya kombe hilo kwa jumla ya goli 4-1.
Jumamosi hii Machi 2 timu hizo zitakutana tena Santiago Bernabeu ambapo hii itakuwa ni mechi ya marudiano ya ligi kuu nchini Hispania La Liga