Ramos afungiwa mechi 2 na UEFA
Beki wa Real Madrid Sergio Ramos amefungiwa mechi mbili za klabu bingwa Ulaya na UEFA kwa kosa la kutafuta kadi ya njano kwa kusudi kwenye mchezo wa kwanza wa hatua ya 16 bora klabu bingwa Ulaya dhidi ya Ajax Februari 13.
Njano hiyo aliyoipata dakika ya 89 ya mchezo huo ambao Real Madrid walishinda kwa goli 2-1, aliitafuta ili kufikisha kadi tatu za njano kwenye michuano hiyo msimu huu hivyo aweze kukosa mechi ya marudiano itakayochezwa Santiago Bernabeu na kurejea akiwa msafi katika hatua ya robo fainali ambapo kuna uwezekano mkubwa wa kukutana na mpinzani mkali.