Mike Dean ahamishiwa majukumu ili kumkwepa Pochettino
Bodi ya waamuzi nchini England imeamua kumuondoa Mike Dean katika nafasi ya mwamuzi wa akiba wa mchezo wa Tottenham Hotspurs dhidi ya Chelsea utakaopigwa Jumatano hii katika uwanja wa Stamford Bridge, mwamuzi huyo ameondolea katika mchezo huo na kupangiwa mchezo mwingine.
Mike Dean ameondolewa katika mchezo huo kwa madai ya sintofahamu yake iliyotokea kati yake ya kocha wa Tottenham Hotspurs Mauricio Pochettino siku ya Jumamosi katika mchezo dhidi ya Burnley uliomalizika kwa Tottenham kupoteza kwa 2-1.
Kutengeneza imani kwa waamuzi wa mchezo huo wa Chelsea na Spurs, ndio bodi ikaamua kumbadilishia majukumu hayo na kumpangia kuwa mwamuzi wa akiba wa mechi ya Manchester City dhidi ya West Ham United ambao pia utapigwa siku ya jumatano.