Mayanja apewa kazi nzito Uganda
Kimya cha mwaka mmoja katika kazi ya ukocha kwa aliyekuwa kocha msaidizi wa klabu ya Simba raia wa Uganda Jackson Mayanja ameripotiwa kupewa mtihani wa kukinoa kikosi ch a Kyetume FC cha Uganda kwa kandarasi ya muda mfupi akiungana na kocha Allan Kabonge.
Jackson Mayanja ambaye ana leseni ya ukocha wa daraja A kutoka shirikisho la mpira wa miguu Afrika, amepewa majukumu ya kukinoa Kyetume FC ili kuiwekwa katika nafasi nzuri ya kuipandisha daraja kutoka Ligi daraja la kwanza hadi kuipeleka Ligi Kuu ya nchini Uganda akishirikiana na mwenzake Kabonge.
Mayanja aliachana na Simba baada ya kudumu kama msaidizi wa makocha kadhaa Simba SC akiwemo Dylan Kerr mwaka 2017 na hakuwa na timu yoyote kwa takribani mwaka mmoja sasa na ndio ameamua kurejea tena mzigoni, Mayanja aliwahi kuwa kocha wa timu mbalimbali kama Lyantonde (URA), Kiyovu, Bunamwaya (Vipers), KCC, Kololo SS, Kagera, Coastal Union, Simba (Tanzania) na pia kuwa kocha msaidizi wa timu ya taifa ya kwao Uganda kwa zaidi ya miaka sita