Kamati ya saidia Taifa Stars yakutana
Baada ya Shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF) kutangaza kamati ya saidia Taifa stars ishinde februari 20 mwaka huu,Kuelekea mchezo wa kuitafuta tiketi ya kucheza Fainali za Afrika 2019 dhidi ya Uganda mwezi Machi kamati hiyo imeanza kufanya kazi leo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Saidia Taifa Stars Ishinde Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda leo Februari 25 amekutana na wajumbe wa Kamati hiyo katika Kikao cha Kwanza kilichofanyika kwenye Hoteli ya Serena,Dar es salaam na kupanga mikakati ya kufanya kwaajili ya Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa stars.
Kamati hiyo ina watu 14 wakiongozwa na Mwenyekiti wao mkuu wa mkoa Paul Makonda, katibu wake akiwa Egn.Heris Said, Mohamed Dewji,Salim Abdallah ‘ try again’ ,Patrick Kahemele,Farouk Barhoza,Mohamed Nassor,Abdallah Bin Kleb,Teddy Mapunda,Haji Manara,Philimon Ntaihaja,Faridi Nahidi,Faraji Asas na Jerry Muro.
Tanzania inashika nafasi ya tatu katika kundi L wakiwa na pointi 5 sawa na Lesotho ambao wapo nafasi ya pili, Uganda wakiwa wamefuzu tayari wakiwa na pointi 13, Cape Verde wakishika nafasi ya nne na pointi 4.
Hivyo Tanzania katika mechi yao hiyo ya mwisho Machi 22 jijini Dar es salaam dhidi ya Uganda, wanatakiwa kuchukua pointi 3 huku wakiombea Lesotho asishinde mechi yake dhidi ya Cape Verde ugenini.