Huu ndio mlango pekee wa kutokea Chelsea
Klabu ya Chelsea kwa sasa ipo katika wakati mgumu kutokana na shirikisho la mpira wa miguu Ulimwenguni FIFA kuifungia kufanya usajili kwa madirisha mawili ya usajili yajayo kwa kosa la kuvunja sheria za usajili kwa wachezaji wa kigeni walio chini ya umri wa miaka 18.
Chelsea wamepigwa faini ya pauni 460000 na FIFA baada ya kupatikana na hatia ya kuvunja sheria hiyo ya usajili , na kama rufaa yao haitakubaliwa basi watajikuta wakitumia wachezaji wale wale waliopo hadi dirisha la usajili la Julai 2020.

Hata hivyo Chelsea watakuwa na nafasi moja pekee ya kuimarisha kikosi chao kama watatumikia adhabu hiyo , nafasi hiyo ni kuwarudisha baadhi ya wachezaji wake inayowamiliki ambao wapo kwa mkopo katika timu nyingine, Chelsea hadi sasa ina wachezaji 41 iliyowatoa kwa mkopo na inaweza kuwarudisha na kuwatumia kwani ni mali yao.
Baadhi ya wachezaji wa Chelsea walio nje kwa mkopo kati ya 41 ni Tammt Abraham (Aston Villa), Ola Aina (Torino), Victorien Agban (Metz), Tiemoue Bakayoko (AC Milan), Michy Batshuayi (Crystal Palace), Nathan Baxter (Yeovil Twon), Izzy Brown (Leeds United), Kylian Hazard (Cercle Brugge), Kenedy (New Castle), Alvaro Morata (Atletico Madrid) Kourt Zouma (Everton), Victor Moses (Fenerbahce) na Christian Pulisic (Borussia Dortmund).