Yanga katika ratiba ngumu tena
Baada ya kurejea jana Jijini Dar es Salaam kutokea Mwanza Mapema asubui ya leo kikosi cha Yanga kimesafiri kuelekea Lindi kwenye mchezo wa kombe la FA dhidi ya Namungo FC utakaochezwa februari 24 mwaka huu siku ya jumapili.
Msafara umejumuisha wachezaji 20,benchi la ufundi wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati ya usajili na Mashindano Hussein Nyika.
Yanga akishatoka mkoani Lindi atarudi tena Mwanza kwaajili ya mchezo wa Ligi kuu dhidi ya Alliance FC utakaochezwa machi 2 mwaka huu katika Uwanja wa CCM Kirumba.