Usaliti wamfanya Martial kuomba msamaha hadharani
Staa wa Man United Anthony Martial ametumia mtandao wa Instagram kuomba msamaha kwa mchumba wake Melania da Cruz kufuatia tuhuma zinazomkabili mchezaji huyo za kumsaliti mpenzi wake wakati akiwa na ujauzito.
Martial,23,aliripotiwa kumsaliti mchumba wake kwa kutoka kimapenzi na mwanamitindo wa Ufaransa Malika Semich mwaka jana mwezi Julai.
.
“ Ningependa kuomba msamaha kwa ndugu zangu, familia yangu na hasa hasa kwa mchumba wangu kwa mabaya niliyofanya miezi ya karibuni.
Nimefanya makosa na nisamehe, haitatokea tena “ Martial aliandika kwenye Instagram.
Ripoti zinasema kuwa Martial alikutana na Melika Semichi katika klabu za usiku kipindi hicho mchumba wake akiwa na ujauzito wa miezi nane.
Kwa mujibu wa mtandao wa Daily Star Sunday, Martial alilala na mwanamitindo huyo mwenye umri wa miaka 20 Paris Hotel.
Martial na mchumba wake, Da Cruz kwa pamoja wana mtoto mmoja wa kiume, anaitwa Swan.
Mchezaji huyo pia ana mtoto mmoja wa kike kutoka katika mahusiano yake ya awali ambapo alizaa na mpenzi wake wa kutoka utotoni Samantha Jacquelinet