Diarra avunja mkataba na PSG
Inawezekana isiwe habari kubwa na kushangaza kwa wadau na mashabiki wa soka barani Ulaya kuhusiana na kiungo wa zamani wa wa Chelsea, Arsenal, Real Madrid ya nchini Hispania na timu ya taifa ya Ufaransa Lassana Diarra kutangaza kufikia makubaliano ya kuvunja mkataba na iliyokuwa klabu yake ya sasa ya Paris Saint Germain ya Ufaransa.
Lassana Diarra ambaye ambaye ametamba na vilabu mbalimbali barani Ulaya kwa uwezo wake aliyouonesha akizitumikia timu hizo, imeripotiwa kuwa alifikia maamuzi ya kuvunja mkataba na PSG toka Februari 2019 akiwa amebakiza miezi kadhaa kumaliza mkataba wake kwa sababu ya kukosa nafasi.
Kiungo huyo kwa sasa ana umri wa miaka 33 lakini toka amewasili Leandro Peredes katika kikosi cha PSG mwezi Januari nafasi yake ya kukitumikia kikosi hicho imezidi kuwa ndogo zaidi licha ya kuwa hadi sasa PSG hawajatoa taarifa rasmi za kuvunjiana mkataba na mchezaji huyo lakini vyanzo vya ndani vimeeleza kuwa Lassana hatoichezea tena timu hiyo.
Lassana ambaye alijiunga na PSG katika kipindi cha usajili cha Januari 2018 kwa kandarasi ya mwaka mmoja na nusu akitokea klabu ya Emrat Club Al Jazira, hadi sasa ameitumikia PSG katika mechi 19 tu na kati ya hizo nne amecheza msimu huu na mara ya mwisho kuichezea ikiwa ni Oktoba 2018 katika ushindi wa PSG wa 5-0 dhidi ya Amiens na mkataba wake wa PSG waliyouvunja kwa mujibu wa onefootball.com kwa makubaliano ya pande zote mbili ulikuwa umalizike June 2019.