Zidane awapa masharti Chelsea
Taarifa zilizosambaa katika mitandao mbalimbali ya michezo barani Ulaya ni kuhusiana na klabu ya Chelsea kupewa masharti na Kocha wa zamani wa Real Madrid Zinedine Zidane ili ajiunge nao kama kocha mkuu mpya wa kikosi hicho, Chelsea ikiwa ina muda mchache na Maurizio Sarri inadaiwa kumuhitaji sana Zidane.
Zidane zimeripotiwa tetesi katika mtandao wa The Sun kuwa ametoa masharti mawili katika klabu ya Chelsea kama kweli inahitaji huduma yake Stamford Bridge, inaelezwa kuwa Zidane ametaka dau la pauni milioni 200 atengewe kwa ajili ya kufanya usajili wa wachezaji ndipo asaini mkataba, pili Chelsea inatakiwa ihakikishe imempa mkataba mpya Eden Hazard ambaye kuna hofu ya kuondoka.
Kama utakuwa unakumbuka vizuri kocha Zinedine Zaidane ambaye hana timu kwa sasa , alijiuzulu nafasi yake ya ukocha Real Madrid kulinda heshima yake baada ya kuweka rekodi ya kutwaa makombe matatu mfululizo ya Klabu Bingwa Ulaya (2016,2017,2018) , wakati Chelsea ikioneshwa bado kutokuwa na imani ya kutosha kwa kocha wake Maurizio Sarri aliyejiunga na timu hiyo Julai 2018 akitokea Napoli ya Italia.