Wizara ya Saudi Arabia yakanusha kuinunua Man United
Baada ya kuenea kwa taarifa katika mitandao ya kijamii kuwa Prince Mohammed Bin Salman wa Saudi Arabia yupo katika mipango ya kutaka kuinunua klabu ya Manchester United ya nchini England, wizara habari ya nchi hiyo kupitia waziri wake imekanusha taarifa kuwa Prince anataka kuinunua klabu hiyo.
Taarifa za Prince Mohammed Bin Salma kutaka kuhusishwa kuinunua klabu hiyo zilizidi kusambaa katika mitandao ya kijamii, baada ya kuonekana viongozi wa juu wa Manchester United wakiwa nchini Saudia na kufanya mazungumzo na Prince Mohammed Bin Salman, kitu ambacho kimekanushwa vikali.
Ukweli wa taarifa zilizotolewa na wizara ya michezo ya nchi hiyo zinaeleza kuwa ni kweli, viongozi wa Manchester United na Prince Mohammed Bin Salman walikutana na kufanya mazungumzo kuhusiana na ishu za kufanya udhamini kupitia shirika la umma la nchi hiyo lakini sio Prince kuinunua timu hiyo.