Marcelo Biesla awaponza Leeds United
Klabu ya Leeds United imetiwa hatiani na wasimamizi wa Ligi ya Champioship nchini England wanaojulikana kwa jina la (EFL), Leeds imetiwa hatiani na kupigwa faini ya pauni 200000 kama fidia baada ya kugundulika kwenda kuwafanyia upepelezi Derby County.
Kwa kawaida hairuhusiwi kwenda katika mazoezi ya mpinzani wako kwenda kufanya upelelezi (spy), hivyo Leeds United wamekutana na rungu hilo baada ya kubaini kuwa kocha wao mkuu Marcelo Bielsa alituma staff wake kwenda kisiri katika mazoezi ya Derby County.
Staff wa Leeds United aliyetumwa na Marcelo Bielsa inaelezwa kuwa alionekana nje ya uwanja wa mazoezi wa timu hiyo, ikiwa ni siku chache kabla ya timu zao kukutana katika mchezo wa Championship uliyokuwa umepangwa kupigwa January 10 2019, Leeds walishinda mechi hiyo kwa goli 2-0.
Marcelo Bielsa, kocha wa Leeds alikiri kuwa amekuwa akifanya upelelezi katika mazoezi ya timu zote Championship msimi huu, ikiwa ni njia yake ya kuiwezesha timu yake kufanya vizuri ili kupanda kuingia ligi kuu nchini England.
Leeds United ambao wanashika nafasi ya tatu katika Championship baada ya kupigwa faini hiyo wamekiri kufuata sheria za EFL ambayo inasema kuwa timu hairuhusiwi kwenda kutizama mazoezi ya timu pinzani saa 72 kabla ya mechi kati yao, labda wawe wamealikwa.