De gea kuweka historia mpya Man United
Kufuatia uwezo mkubwa anaoendelea kuuonesha mlinda mlango wa Manchester United raia wa Hispania David De Gea katika michezo mbalimbali akiendelea kuitumikia timu hiyo, umekuwa gumzo mitandaoni kiasi cha kupokea sifa nyingi kila kona kuanzia kwa mashabiki hadi wachambuzi wa soka duniani kote.
Klabu ya Manchester United ambayo inamshawishi David De Gea aendelee nao, imeripotiwa kuwa tayari kumfanya aingie kwenye vitabu vya kumbukumbu ya kuwa mchezaji pekee anayelipwa mshahara mkubwa Manchester United, David De Gea ameripotiwa kuwa endapo atasaini mkataba mpya atalipwa mshahara wa pauni 365,000 ( Tsh Bilioni 1.1) kwa wiki na kuwazidi mchezaji mwenzake Alex Sanchez na Mesut Ozil wa Arsenal.
Hivyo dau hilo litamuweka mchezaji huyo katika rekodi ya kuwa mchezaji mwenye mshahara mkubwa zaidi kwa sasa nchini England, kwani hakuna mchezaji anayelipwa mshahara huo England kwa sasa.
De Gea toka ajiunge na Manchester United 2011 akitokea Atletico Madrid ya kwao Hispania, amecheza jumla ya mechi 263, mechi 99 bila kuruhusu goli, akiiongoza Manchester United kushinda michezo 152 na kupoteza michezo 52.