Serengeti Boys waendelea kujifua
Timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17, Serengeti Boys inaendelea kujifua kwenye Uwanja wa Aghakhan Jijini Arusha kwaajili ya kujiandaa na Fainali za Afrika kwa vijana U17.
Akizungumza na Worldsports14 Msemaji wa Shirikisho la Soka nchini Clifford Mario Ndimbo amesema kuwa wachezaji 31 walioko Kambini jijini Arusha wanaendelea vizuri kiafya na kufanya mazoezi.
” Timu ipo Arusha ilikoweka Kambi huko na wachezaji wote wanaendelea vizuri kiafya na leo asubuhi wamefanya mazoezi kwenye viwanja vya Aghakhan vilivyopo mjini humo” amesema Ndimbo
Fainali hizo zitakazofanyika mwezi April mwaka huu na Tanzania ikiwa ni mwenyeji wa michuano hiyo.