Fei Toto na Gadiel Michael kuwakosa Mbao
Wachezaji wawili wa Klabu ya Yanga ambae ni Kiungo Feisal Salum” fei Toto ” na Beki Gadiel Michael wataukosa mchezo wa Ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Mbao FC ya Mwanza kwa kuwa na kadi tatu za njano.
Mchezo huo utachezwa februari 20 mwaka huu (jumatano) katika Uwanja wa CCCM kirumba Jijini Mwanza.
Mratibu wa Klabu ya Yanga Hafidhi Salehe amesema kuwa katika mchezo huo watawakosa wachezaji hao ambao ni muhimu katika kikosi chao kutokana na kuwa na kadi hizo.
.
” Tutawakosa wachezaji wetu wawili Fei Toto na Gadiel Michael ambao ni muhimu sana katika kikosi chetu kwa sababu wana kadi tatu za njano hivyo hawatakuwa sehemu ya mchezo wa jumatano, pia tunamshukuru Mungu tumefika salama Mwanza na timu itafanya mazoezi leo jioni kwenye Uwanja wa CCM Kirumba hapa Mwanza ” amesema Hafidhi.
Yanga anakutana na Mbao akiwa amecheza michezo 24 na anashika nafasi ya kwanza katika msimamo wa Ligi akiwa na point 58 huku mpinzani wake Mbao FC akiwa amecheza michezo 26 akishika nafasi ya 6 na point 36.