Mbadala wa Ozil wapatikana Ujerumani
Wakati kukiwa na sintofahamu kuhusiana na hatma ya kiungo wa kimataifa wa Ujerumani mwenye asili ya Uturuki Mesut Ozil kuwa anaweza kuondoka katika timu ya Arsenal kwa madai ya kukosa furaha lakini anaonekana kuwa kama sio chaguo namba moja la kocha mpya wa timu hiyo Unai Emery.
Zimeripotiwa taarifa mpya klabu ya Arsenal inajipanga kumleta mrithi wa Mesut Ozil katika timu hiyo, kwa mujibu wa tetesi zinazosambaa katika mitandao mingi ya habari za michezo Ulaya ni kuwa Arsenal wamejipanga kutaka kumsajili kiungo wa Bayer Leverkusen ya Ujerumani Kai Havertz.
Kai Havertz mwenye umri wa miaka 19 kwa sasa anatazamiwa kwenda kuwa mbadala sahihi wa Mesut Ozil ambaye inaonekana kama sio chaguo la kocha Unai Emery.
Havertz ambaye anafananisha na Toni Kroos, amekuwa gumzo katika bundesliga msimu huu, ambapo katika mechi 21 alizocheza za ligi hiyo amefunga magoli 8 na huku akifunga mengine matatu katika Europa ligi.
Lakini si magoli hayo ambayo yamewashika Arsenal kumuwinda kiungo huyo, ila ni aina yake ya uchezaji ambapo anacheza katika nafasi ya kiungo anayechezesha timu, akiwa pia ametoa jumla ya assist sita.
Miamba ya La Liga Barcelona na Real Madrid pia wanamtolea macho.
Endapo The Gunners watamnasa itakuwa safari ya Mesut Ozill imewadia.
Ozil ambaye ana umri wa miaka 30 ndiye mchezaji wa Arsenal anayelipwa zaidi Pauni 350,000 kwa wiki ( Tsh Bilioni 1 ).